Neno Kutoka kwa Askofu

Neno la Mungu linabainisha kuwa kanisa ni mwili wa Kristo (Efe 1:22-23). Maana yake ni kwamba mahali lilipo kanisa la kweli hapo hapo Kristo yupo. Yeye ni mtawala wa mioyo ya wakristo wa kweli ndani ya kanisa na anaonekana katika jamii kupita maisha yao. Yuko tayari kuihudumia jamii na wanadamu kupitia kanisa. Hivyo shughuri ya kuanzisha kanisa katika jamii ambamo hakuna kanisa ni kushiriki katika tendo la Kristo kushuka na kuja kuishi katika jamii. Jambo hilo ni nafasi ya pekee na muhimu ya kumtumikia Bwana.

Siyo wakristo wengi, au hata watumishi wengi, waliojaliwa binafsi fursa ya kushiriki katika tendo la Kristo kushuka katika jamii mpya. Lakini wale waliokwisha kushiriki katika tendo la Kristo kushuka katika jamii wanafahamu kuwa siyo jambo rahisi. Ni jambo linalohitaji kuomba na kuombewa, linahitaji kujifunza na kufundishwa. Ni jambo linalohitaji utii, nidham na unyenyekevu.

Sisi wakristo wa Dayosisi ya Tabora tumejaliwa kupata fursa kubwa ya kushiriki katika kazi ya Kristo kushuka katika jamii mbali mbali kuanzisha mwili wake. Tumenyenyekezwa mno katika kufanya kazi pamoja naye akianzisha mwili wake katika jamii mbalimbali (1Kor 3:9). Yeye ametufunza mambo mengi. Ametufunza kutokwenda na utaratibu wetu uliuo tayari kutumiwa mara moja. Baali tunahitaji kumwomba kila mara atuonyeshe njia yake. Anataka utii wetu.

Tunawashukuru wote walioshirikiana nasi katika kazi hii ya kwenda pamoja na Kristo kuanzisha mwali wake katika jamii mbali mbali. Kwa msingi wa Warumi 10:13-17, sote tukishiriki pamoja na Kristo akianzisha mwili wake katika jamii mbali mbali. Mungu awabariki nyote. Amina’

A word from the Bishop

The Word of God affirms that the Church is the body of Christ (Ephesians 1:22-23). This means where there is a Church Christ is there among the believers. He is the Ruler of the hearts the true believers and He is visible in the community through their lives. He is prepared to serve the community through the Church. So the task of planting a new church in a community is participating in Christ’s chore of coming to dwell with His people. This is a special opportunity to serve Him.

Not many believers or ministers have personally been privileged to participate in Christ’s task of coming in a community to build His Church. Nevertheless, those who had had that privilege to do so know how difficult it is. It requires praying and being prayers from brethren, it requires learning and being a keen learner. It requires obedience, discipline and submissiveness.

We believers of Tabora Diocese have been given a big opportunity to participate in the Christ’s task of coming to various communities to establish His body. We have been humbled to work with Him in many communities as He establishes His body (1 Corinthians 3:9). He has taught us many things. Above all, He has taught us not to accompany Him with our ready-made formats and premeditated answers. He wants us to ask Him every step we move. He wants our obedience.

We thank all those who helped us in one way or another. Based on Romans 10:13-17, we were all together accompanying Christ as He established His body in the communities. May God Bless all of you.Amen